Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.
1 Wakorintho 2:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilifanya hivyo kusudi imani yenu ipate kutegemea nguvu ya Mungu, na si hekima ya binadamu. Biblia Habari Njema - BHND Nilifanya hivyo kusudi imani yenu ipate kutegemea nguvu ya Mungu, na si hekima ya binadamu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilifanya hivyo kusudi imani yenu ipate kutegemea nguvu ya Mungu, na si hekima ya binadamu. Neno: Bibilia Takatifu ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu. BIBLIA KISWAHILI ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. |
Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.
Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika.
Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu.
katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kulia na za mkono wa kushoto;