Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
1 Wakorintho 15:57 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Biblia Habari Njema - BHND Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Mungu apewe shukrani, yeye atupaye ushindi kupitia kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Isa Al-Masihi. BIBLIA KISWAHILI Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. |
Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
Sasa mwanangu, BWANA na awe pamoja nawe; ukafanikiwe, na kuijenga nyumba ya BWANA, Mungu wako, kama alivyonena kuhusu habari zako.
Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kulia, Na mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Alipokwisha kusema hayo akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula.
Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.
Lakini katika mambo hayo yote sisi ni zaidi ya washindi, kupitia kwake yeye aliyetupenda.
ninyi nanyi mkisaidiana nasi kwa ajili yetu katika kuomba, ili, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa msaada wa watu wengi, watu wengi watoe shukrani kwa ajili yetu.
Ila Mungu ashukuriwe, anayetufanya tushangilie ushindi daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.