Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.
1 Wakorintho 15:56 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kifo hupata sumu yake katika dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika sheria. Biblia Habari Njema - BHND Kifo hupata sumu yake katika dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika sheria. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kifo hupata sumu yake katika dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika sheria. Neno: Bibilia Takatifu Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria. Neno: Maandiko Matakatifu Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria. BIBLIA KISWAHILI Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. |
Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.
Basi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi hamuwezi kuja.
Kwa hiyo niliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.
Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.
Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.
Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.