1 Wakorintho 15:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema na kama Kristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayana maana na imani yenu haina maana. Biblia Habari Njema - BHND na kama Kristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayana maana na imani yenu haina maana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza na kama Kristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayana maana na imani yenu haina maana. Neno: Bibilia Takatifu Tena ikiwa Al-Masihi hakufufuliwa kutoka kwa wafu, kuhubiri kwetu kumekuwa ni bure na imani yenu ni batili. Neno: Maandiko Matakatifu Tena ikiwa Al-Masihi hakufufuliwa kutoka kwa wafu, kuhubiri kwetu kumekuwa ni bure na imani yenu ni batili. BIBLIA KISWAHILI tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. |
Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina BWANA, na thawabu yangu ina Mungu wangu.
Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.
na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiria isipokuwa mliamini bure.
Nami nilikwenda kwa kuwa nilifunuliwa, nikawaeleza Injili ile niihubiriyo katika Mataifa, lakini kwa faragha kwa hao viongozi waliosifika, isiwe labda napiga mbio bure, au nilipiga mbio bure.
Maana, ikiwa tunaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, ili hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.