Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda.
1 Wakorintho 13:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote. Biblia Habari Njema - BHND Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote. Neno: Bibilia Takatifu Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote. Neno: Maandiko Matakatifu Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote. BIBLIA KISWAHILI huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. |
Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda.
Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.
Kwa maana tuliokolewa kwa tumaini; lakini kitu kilichotumainiwa kikionekana, hakiwi tumaini tena. Kwa maana ni nani anayekitumainia kile akionacho?
Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo.
Hata na sisi wenyewe tunaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya subira yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili.
Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;
na upendo, na subira; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.
Bali wewe, uwe mwenye kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza huduma yako kwa ukamilifu.
Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji la uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.