Nawe utawaambia watu wote wenye uwezo wa hali ya juu, niliowapa ubingwa wamfanyie Haruni mavazi ili awekwe wakfu anitumikie katika kazi ya ukuhani.
1 Wakorintho 12:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida ya wote. Biblia Habari Njema - BHND Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida ya wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida ya wote. Neno: Bibilia Takatifu Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho wa Mungu kwa faida ya wote. Neno: Maandiko Matakatifu Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote. BIBLIA KISWAHILI Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. |
Nawe utawaambia watu wote wenye uwezo wa hali ya juu, niliowapa ubingwa wamfanyie Haruni mavazi ili awekwe wakfu anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.
Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, jitahidini kusudi mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa.
lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, kuliko kunena maneno elfu kumi kwa lugha.
Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kutoa unabii, maana yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.