1 Wakorintho 12:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile tunavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi, Biblia Habari Njema - BHND Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi, Neno: Bibilia Takatifu Navyo vile viungo tunavyoviona havina heshima, ndivyo tunavipa heshima maalum. Vile viungo vya mwili ambavyo havina uzuri, tunavipa heshima ya pekee; Neno: Maandiko Matakatifu Navyo vile viungo tunavyoviona havina heshima, ndivyo tunavipa heshima maalum. Vile viungo vya mwili ambavyo havina uzuri, tunavipa heshima ya pekee; BIBLIA KISWAHILI Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile tunavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. |
Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajitambua kuwa wako uchi, wakashona majani ya mtini, na kujifanyia mavazi ya kusitiri uchi wao.
Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vinahitajiwa zaidi.
Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa;
Lakini ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;