Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
1 Wakorintho 12:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote – ingawaje ni vingi – hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo. Biblia Habari Njema - BHND Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote – ingawaje ni vingi – hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote — ingawaje ni vingi — hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo. Neno: Bibilia Takatifu Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi; navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Al-Masihi. Neno: Maandiko Matakatifu Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi, navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Al-Masihi. BIBLIA KISWAHILI Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. |
Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
Basi ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazawa, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo.
kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;
Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake;
wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukineemeshwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kama atakavyo Mungu.
Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.