Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.
1 Wakorintho 10:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi kushiriki katika Karamu ya Bwana na katika meza ya pepo. Biblia Habari Njema - BHND Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi kushiriki katika Karamu ya Bwana na katika meza ya pepo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi kushiriki katika Karamu ya Bwana na katika meza ya pepo. Neno: Bibilia Takatifu Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana Isa na cha mashetani pia. Hamwezi kuwa na sehemu katika Chakula cha Bwana Isa na katika chakula cha mashetani pia. Neno: Maandiko Matakatifu Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana Isa na cha mashetani pia. Hamwezi kuwa na sehemu katika chakula cha Bwana Isa na katika chakula cha mashetani pia. BIBLIA KISWAHILI Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. |
Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.
Bali ninyi mmwachao BWANA, na kuusahau mlima wangu mtakatifu, na kuandaa meza kwa ajili ya Bahati, na kuijazia Ajali vyombo vya divai iliyochanganyika;
kwa kuwa mnanikasirisha kwa matendo ya mikono yenu, mkifukizia uvumba miungu mingine katika nchi ya Misri, mlikokwenda kukaa ugenini; mpate kukatiliwa mbali, na kuwa laana, na aibu, katika mataifa yote ya dunia?
Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
Kwa maana, mtu akikuona wewe uliye na ujuzi, umeketi chakulani ndani ya hekalu la sanamu, je! Dhamiri yake mtu huyo, kwa kuwa yuko dhaifu, haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?