1 Wakorintho 1:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mwenye kutaka kujivuna, na ajivunie kazi ya Bwana.” Biblia Habari Njema - BHND Basi, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mwenye kutaka kujivuna, na ajivunie kazi ya Bwana.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mwenye kutaka kujivuna, na ajivunie kazi ya Bwana.” Neno: Bibilia Takatifu Hivyo, kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Mwenyezi Mungu.” Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo, kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana Mwenyezi.” BIBLIA KISWAHILI kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana. |
Nanyi semeni, Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako.
Utawapepeta, na upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfurahia BWANA, utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli.
nawe utaapa hivi, Kama BWANA aishivyo, katika kweli, na katika hukumu, na katika haki ndipo mataifa watabarikiwa na yeye, nao watajitukuza katika yeye.
Kwa maana ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu.
Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.
Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.