1 Wakorintho 1:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, hakuna mtu awezaye kujivunia chochote mbele ya Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, hakuna mtu awezaye kujivunia chochote mbele ya Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, hakuna mtu awezaye kujivunia chochote mbele ya Mungu. Neno: Bibilia Takatifu ili mtu yeyote asijisifu mbele zake. Neno: Maandiko Matakatifu ili mtu yeyote asijisifu mbele zake. BIBLIA KISWAHILI mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. |
Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti.
BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;
Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;
Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani.
Kwa maana ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu.
Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?