1 Wafalme 9:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akasema, Miji gani hii uliyonipa, ndugu yangu? Akaiita nchi ya Kabuli, hata leo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, akamwuliza Solomoni, “Ndugu yangu, ni miji gani hii ambayo umenipa?” Ndio sababu miji hiyo inaitwa nchi ya Kabuli hata leo. Biblia Habari Njema - BHND Basi, akamwuliza Solomoni, “Ndugu yangu, ni miji gani hii ambayo umenipa?” Ndio sababu miji hiyo inaitwa nchi ya Kabuli hata leo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, akamwuliza Solomoni, “Ndugu yangu, ni miji gani hii ambayo umenipa?” Ndio sababu miji hiyo inaitwa nchi ya Kabuli hata leo. Neno: Bibilia Takatifu Hiramu akauliza, “Hii ni miji ya namna gani uliyonipa, ndugu yangu?” Naye akaiita nchi ya Kabul, jina lililoko hadi leo. Neno: Maandiko Matakatifu Hiramu akauliza, “Hii ni miji ya namna gani uliyonipa, ndugu yangu?” Naye akaiita nchi ya Kabul, jina lililoko hadi leo. BIBLIA KISWAHILI Akasema, Miji gani hii uliyonipa, ndugu yangu? Akaiita nchi ya Kabuli, hata leo. |
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Tiro, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameitia kabila nzima katika mikono ya Edomu, wala hawakulikumbuka agano la udugu;
kisha ukazunguka kuelekea maawio ya jua mpaka Beth-dagoni, nao ukafikia hadi Zabuloni, tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hadi Bethemeki na Neyeli; kisha ukatokea hadi Kabuli upande wa kushoto;