1 Wafalme 8:49 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC basi, uyasikie maombi yao na dua yao, huko mbinguni, makao yako, ukaitetee haki yao; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema basi, nakusihi kutoka huko mbinguni uliko usikie sala yao na ombi lao uwapatie haki zao. Biblia Habari Njema - BHND basi, nakusihi kutoka huko mbinguni uliko usikie sala yao na ombi lao uwapatie haki zao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza basi, nakusihi kutoka huko mbinguni uliko usikie sala yao na ombi lao uwapatie haki zao. Neno: Bibilia Takatifu basi usikie dua na maombi yao ukiwa mbinguni, makao yako, ukawape haki yao. Neno: Maandiko Matakatifu basi kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, usikie dua yao na maombi yao na kuitetea haki yao. BIBLIA KISWAHILI basi, uyasikie maombi yao na dua yao, huko mbinguni, makao yako, ukaitetee haki yao; |
watakaporejea kwako kwa mioyo yao yote, na kwa nia zao zote, katika nchi ya adui zao, waliowachukua mateka, wakikuomba, kwa kuikabili nchi yao, uliyowapa baba zao, na mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako;
ukawasamehe watu wako waliokutenda dhambi, na makosa yao yote waliyokukosa; ukawape kuonewa huruma mbele yao waliowachukua mateka, ili wapate kuwahurumia.
Basi sasa, Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe na mkono wake, nakusihi, ili kwamba falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe BWANA Mungu, wewe peke yako.