Akavileta vile vitu alivyovitakasa baba yake, na vile alivyovitakasa yeye mwenyewe, katika nyumba ya BWANA, fedha; na dhahabu, na vyombo.
1 Wafalme 7:51 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hivyo kazi yote aliyoifanya mfalme Sulemani katika nyumba ya BWANA ikamalizika. Sulemani akaviingiza vile vitu alivyovitakasa Daudi baba yake, yaani, fedha, na dhahabu, na vyombo; akavitia ndani ya hazina za nyumba ya BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, mfalme Solomoni akamaliza kazi zote zilizohusu nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Kisha Solomoni akaleta mali yote ambayo baba yake Daudi, alikuwa ameiweka wakfu, yaani: Fedha, dhahabu na vyombo; akaiweka katika hazina za nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, mfalme Solomoni akamaliza kazi zote zilizohusu nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Kisha Solomoni akaleta mali yote ambayo baba yake Daudi, alikuwa ameiweka wakfu, yaani: Fedha, dhahabu na vyombo; akaiweka katika hazina za nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, mfalme Solomoni akamaliza kazi zote zilizohusu nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Kisha Solomoni akaleta mali yote ambayo baba yake Daudi, alikuwa ameiweka wakfu, yaani: fedha, dhahabu na vyombo; akaiweka katika hazina za nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo, Mfalme Sulemani alipomaliza kazi zote za Hekalu la Mwenyezi Mungu, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo Mfalme Sulemani alipomaliza kazi ya Hekalu la bwana, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: yaani fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la bwana. BIBLIA KISWAHILI Hivyo kazi yote aliyoifanya mfalme Sulemani katika nyumba ya BWANA ikamalizika. Sulemani akaviingiza vile vitu alivyovitakasa Daudi baba yake, yaani, fedha, na dhahabu, na vyombo; akavitia ndani ya hazina za nyumba ya BWANA. |
Akavileta vile vitu alivyovitakasa baba yake, na vile alivyovitakasa yeye mwenyewe, katika nyumba ya BWANA, fedha; na dhahabu, na vyombo.
Basi ndivyo alivyoijenga nyumba, akaimaliza; akaifunika nyumba kwa boriti na mbao za mwerezi.
Na vyetezo, na mabakuli; vilivyokuwa vya dhahabu katika dhahabu, na vilivyokuwa vya fedha katika fedha, kamanda wa askari walinzi akavichukua.
Hivyo ikaisha kazi yote Sulemani aliyoifanyia nyumba ya BWANA. Sulemani akaviingiza vitu alivyovitakasa baba yake Daudi; fedha, na dhahabu, na vyombo vyote, akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Mungu.
Wala hawakuyaacha maagizo ya mfalme aliyowaamuru makuhani na Walawi kwa neno lolote, wala kwa habari ya hazina.
Nyumba hiyo ikamalizika siku ya tatu ya mwezi Adari, katika mwaka wa sita wa kutawala kwake mfalme Dario.
Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.
Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu.