Akafanya birika kumi za shaba; birika moja huingia bathi arubaini; na kila birika ilikuwa mikono minne; birika moja juu ya kitako kimoja, katika vile vitako kumi.
1 Wafalme 7:39 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akaviweka vile vitako, vitano upande wa kulia wa nyumba, na vitano upande wa kushoto wa nyumba; akaiweka ile bahari upande wa kulia wa nyumba upande wa mashariki, kuelekea kusini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akaweka magari matano upande wa kusini wa nyumba, na matano upande wa kaskazini; na lile tangi akaliweka kwenye pembe ya kusini-mashariki ya nyumba. Biblia Habari Njema - BHND Akaweka magari matano upande wa kusini wa nyumba, na matano upande wa kaskazini; na lile tangi akaliweka kwenye pembe ya kusini-mashariki ya nyumba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akaweka magari matano upande wa kusini wa nyumba, na matano upande wa kaskazini; na lile tangi akaliweka kwenye pembe ya kusini-mashariki ya nyumba. Neno: Bibilia Takatifu Aliweka vitako vitano upande wa kusini wa Hekalu na vingine vitano upande wa kaskazini. Akaweka ile Bahari upande wa kusini, katika pembe ya kusini-mashariki ya Hekalu. Neno: Maandiko Matakatifu Aliweka vitako vitano upande wa kusini wa Hekalu na vingine vitano upande wa kaskazini. Akaweka ile bahari upande wa kusini, katika pembe ya kusini ya Hekalu. BIBLIA KISWAHILI Akaviweka vile vitako, vitano upande wa kulia wa nyumba, na vitano upande wa kushoto wa nyumba; akaiweka ile bahari upande wa kulia wa nyumba upande wa mashariki, kuelekea kusini. |
Akafanya birika kumi za shaba; birika moja huingia bathi arubaini; na kila birika ilikuwa mikono minne; birika moja juu ya kitako kimoja, katika vile vitako kumi.
Tena Huramu akazifanya birika, na majembe, na mabakuli. Hivyo Huramu akazimaliza kazi zote alizomfanyia mfalme Sulemani katika nyumba ya BWANA;
Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea.
Alivitengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu, kama vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kulia, na vitano upande wa kushoto.
Hivyo ikaisha kazi yote Sulemani aliyoifanyia nyumba ya BWANA. Sulemani akaviingiza vitu alivyovitakasa baba yake Daudi; fedha, na dhahabu, na vyombo vyote, akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Mungu.