Huyo Sulemani akafanya ujamaa na Farao, mfalme wa Misri, akamwoa binti yake Farao, akamleta mjini mwa Daudi, hata alipokwisha kuijenga nyumba yake, na nyumba ya BWANA, na ukuta wa kuuzunguka Yerusalemu.
1 Wafalme 7:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye Sulemani alikuwa katika kuijenga nyumba yake mwenyewe miaka kumi na mitatu, akaimaliza nyumba yake yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Solomoni alijijengea ikulu, nayo ilimchukua miaka kumi na mitatu kumalizika. Biblia Habari Njema - BHND Solomoni alijijengea ikulu, nayo ilimchukua miaka kumi na mitatu kumalizika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Solomoni alijijengea ikulu, nayo ilimchukua miaka kumi na mitatu kumalizika. Neno: Bibilia Takatifu Ilimchukua Sulemani miaka kumi na tatu kukamilisha ujenzi wa jumba lake la kifalme. Neno: Maandiko Matakatifu Ilimchukua Sulemani miaka kumi na mitatu kukamilisha ujenzi wa Jumba lake la kifalme. BIBLIA KISWAHILI Naye Sulemani alikuwa katika kuijenga nyumba yake mwenyewe miaka kumi na mitatu, akaimaliza nyumba yake yote. |
Huyo Sulemani akafanya ujamaa na Farao, mfalme wa Misri, akamwoa binti yake Farao, akamleta mjini mwa Daudi, hata alipokwisha kuijenga nyumba yake, na nyumba ya BWANA, na ukuta wa kuuzunguka Yerusalemu.
Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
Ikawa Sulemani alipokwisha kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, na mambo yote yaliyoingia moyoni mwake Sulemani, naye akataka kuyafanya,
Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani alizijenga zile nyumba mbili, nyumba ya BWANA na nyumba yake mfalme,
Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani aliijenga nyumba ya BWANA, na nyumba yake mwenyewe;