Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
1 Wafalme 6:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Sulemani akaijenga hiyo nyumba akaimaliza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo, Solomoni akaijenga nyumba na kuimaliza. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo, Solomoni akaijenga nyumba na kuimaliza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo, Solomoni akaijenga nyumba na kuimaliza. Neno: Bibilia Takatifu Basi Sulemani akajenga Hekalu na kulikamilisha. Neno: Maandiko Matakatifu Basi Sulemani akajenga Hekalu na kulikamilisha. BIBLIA KISWAHILI Basi Sulemani akaijenga hiyo nyumba akaimaliza. |
Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
Basi ndivyo alivyoijenga nyumba, akaimaliza; akaifunika nyumba kwa boriti na mbao za mwerezi.
Hivyo kazi yote aliyoifanya mfalme Sulemani katika nyumba ya BWANA ikamalizika. Sulemani akaviingiza vile vitu alivyovitakasa Daudi baba yake, yaani, fedha, na dhahabu, na vyombo; akavitia ndani ya hazina za nyumba ya BWANA.
Na mara tatu kila mwaka Sulemani alikuwa akitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu aliyomjengea BWANA akafukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu iliyokuwako mbele za BWANA. Hivyo akaimaliza nyumba.
Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.