Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki.
1 Wafalme 4:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alitunga methali 3,000 na nyimbo 1,500. Biblia Habari Njema - BHND Alitunga methali 3,000 na nyimbo 1,500. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alitunga methali 3,000 na nyimbo 1,500. Neno: Bibilia Takatifu Akanena mithali elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano (1,005). Neno: Maandiko Matakatifu Akanena mithali 3,000 na nyimbo zake zilikuwa 1,005. BIBLIA KISWAHILI Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. |
Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki.
Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wowote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.
Lakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akachunguza, akatunga mithali nyingi.
ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu kuumbwa kwa ulimwengu.