Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




1 Wafalme 4:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Na vyakula vya Sulemani vya siku moja vilikuwa kori thelathini za unga mzuri, na kori sitini za ngano,

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Chakula alichohitaji Solomoni kwa siku moja, kilikuwa unga laini madebe 360, na unga wa kawaida madebe 720,

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Chakula alichohitaji Solomoni kwa siku moja, kilikuwa unga laini madebe 360, na unga wa kawaida madebe 720,

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Chakula alichohitaji Solomoni kwa siku moja, kilikuwa unga laini madebe 360, na unga wa kawaida madebe 720,

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mahitaji ya Sulemani ya kila siku yalikuwa kori thelathini za unga laini, kori sitini za unga wa kawaida.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Mahitaji ya Sulemani ya kila siku yalikuwa kori thelathini za unga laini, kori sitini za unga wa kawaida.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na vyakula vya Sulemani vya siku moja vilikuwa kori thelathini za unga mzuri, na kori sitini za ngano,

Tazama sura
Tafsiri zingine



1 Wafalme 4:22
10 Marejeleo ya Msalaba  

na chakula cha mezani pake, na maofisa wake walivyokaa, na kuhudumu kwao wahudumu wake, na mavazi yao, na wanyweshaji wake, na sadaka zake za kuteketezwa ambazo alizitoa katika nyumba ya BWANA, roho yake ilizimia.


Sulemani akatawala juu ya falme zote, toka Mto mpaka nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri; walimletea tunu, na kumtumikia Sulemani siku zote za maisha yake.


na ng'ombe kumi walionona, na ng'ombe ishirini za malisho, na kondoo mia moja, pamoja na ayala, na paa, na kulungu, na kuku walionona.


Sulemani akampa Hiramu kori elfu ishirini za ngano, chakula cha watu wake, na kori ishirini za mafuta safi. Ndizo Sulemani alizompa Hiramu mwaka kwa mwaka.


na vyakula vya mezani mwake, na kikao cha maofisa wake, na huduma ya watumishi wake na mavazi yao; pia wanyweshaji wake na mavazi yao; na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya BWANA; roho yake ilizimia.


Basi, maandalizi ya chakula yaliyoandaliwa kila siku yalikuwa ng'ombe mmoja na kondoo sita wazuri; tena nikaandaliwa kuku, na mara moja katika siku kumi akiba ya mvinyo ya namna zote; wala kwa hayo yote sikudai marupurupu ya chakula cha mtawala, kwa kuwa watu walikuwa wamebeba mzito mzito.


Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza.


Mali yakiongezeka, hao walao nao wanaongezeka na mwenyewe hufaidiwa nini, ila kuyatazama kwa macho yake tu?


Huyo mfalme akawaagizia wapewe chakula kama cha mfalme, na divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme.


Naye atawaweka kwake kuwa wakuu juu ya maelfu, na makamanda juu ya hamsini hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.