Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

1 Wafalme 20:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Mfalme wa Israeli akajibu, akasema, Mwambieni, Avaaye asijisifu kama avuaye.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mfalme Ahabu wa Israeli akajibu, “Mwambieni mfalme Ben-hadadi kwamba shujaa hujisifu baada ya vita, si kabla!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mfalme Ahabu wa Israeli akajibu, “Mwambieni mfalme Ben-hadadi kwamba shujaa hujisifu baada ya vita, si kabla!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mfalme Ahabu wa Israeli akajibu, “Mwambieni mfalme Ben-hadadi kwamba shujaa hujisifu baada ya vita, si kabla!”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mfalme wa Israeli akajibu, “Mwambieni, ‘Yule anayevaa mavazi ya vita asije akajisifu kama yule anayevua.’ ”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Mfalme wa Israeli akajibu, “Mwambieni, ‘Yule anayevaa mavazi ya vita asije akajisifu kama yule anayevua.’ ”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Mfalme wa Israeli akajibu, akasema, Mwambieni, Avaaye asijisifu kama avuaye.

Tazama sura
Tafsiri zingine

1 Wafalme 20:11
12 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Wamoabi wote waliposikia ya kuwa wafalme hao wamekwea ili kupigana nao, walijikusanya pamoja, wote wawezao kuvaa silaha, na wenye umri zaidi, wakasimama mpakani.

Mwekee mkono wako; Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena.

Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja.

Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.

Wakalia huko, Farao, mfalme wa Misri, ni kishindo tu; muda alioandikiwa ameuacha upite.

BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;

Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya jogoo kuwika, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.

Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyembebea silaha zake, Haya! Na twende tukavuke ngomeni mwa hao wasiotahiriwa; yamkini BWANA atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia BWANA asiokoe, kama ni kwa wengi au kama ni kwa wachache.