Ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaambia; (basi Wagibeoni si wa wana wa Israeli, ila ni wa masalio ya Waamori; na wana wa Israeli walikuwa wamewaapia; lakini Sauli akajaribu kuwaua kwa ari kwa ajili ya wana wa Israeli na Yuda;)
1 Wafalme 2:43 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mbona basi hukukishika kiapo chako kwa BWANA, na amri niliyokuagiza? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mbona basi, umevunja kiapo chako kwa Mwenyezi-Mungu na kutojali amri niliyokupa?” Biblia Habari Njema - BHND Mbona basi, umevunja kiapo chako kwa Mwenyezi-Mungu na kutojali amri niliyokupa?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mbona basi, umevunja kiapo chako kwa Mwenyezi-Mungu na kutojali amri niliyokupa?” Neno: Bibilia Takatifu Kwa nini basi hukutunza kiapo chako kwa Mwenyezi Mungu na kutii amri niliyokupa?” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa nini basi hukutunza kiapo chako kwa bwana na kutii amri niliyokupa?” BIBLIA KISWAHILI Mbona basi hukukishika kiapo chako kwa BWANA, na amri niliyokuagiza? |
Ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaambia; (basi Wagibeoni si wa wana wa Israeli, ila ni wa masalio ya Waamori; na wana wa Israeli walikuwa wamewaapia; lakini Sauli akajaribu kuwaua kwa ari kwa ajili ya wana wa Israeli na Yuda;)
Basi, mfalme akatuma watu, akamwita Shimei, akamwambia, Je! Sikukuapisha kwa BWANA, na kukushuhudia, kusema, Siku ile utakapotoka ukaenda mahali popote, ujue kwamba hakika utakufa? Nawe ukaniambia, Neno hili nililolisikia ni jema?
Tena, mfalme akamwambia Shimei, Umejua uovu wote uliouona moyoni mwako, uliomtenda Daudi baba yangu; basi kwa hiyo BWANA atakurudishia uovu wako kichwani pako mwenyewe.
Tena katika Yuda mkono wa Mungu ulikuwa ukiwapa moyo mmoja, waitimize amri ya mfalme na wakuu kwa neno la BWANA.
Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri.