Akasema, Nakusihi nena na Sulemani, mfalme (kwa kuwa hawezi kukukatalia neno), kwamba anioze Abishagi, Mshunami.
1 Wafalme 2:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye Bathsheba akasema, Vema; nitasema na mfalme kwa ajili yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bathsheba akamwambia, “Sawa; nitazungumza na mfalme kwa niaba yako.” Biblia Habari Njema - BHND Bathsheba akamwambia, “Sawa; nitazungumza na mfalme kwa niaba yako.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bathsheba akamwambia, “Sawa; nitazungumza na mfalme kwa niaba yako.” Neno: Bibilia Takatifu Bathsheba akamjibu, “Vema sana, nitazungumza na mfalme kwa ajili yako.” Neno: Maandiko Matakatifu Bathsheba akamjibu, “Vema sana, nitazungumza na mfalme kwa ajili yako.” BIBLIA KISWAHILI Naye Bathsheba akasema, Vema; nitasema na mfalme kwa ajili yako. |
Akasema, Nakusihi nena na Sulemani, mfalme (kwa kuwa hawezi kukukatalia neno), kwamba anioze Abishagi, Mshunami.
Basi Bathsheba akaingia kwa mfalme Sulemani, aseme naye kwa ajili ya Adonia. Naye mfalme akainuka kwenda kumlaki, akamwinamia, akaketi katika kiti chake cha enzi; kisha akaagiza awekewe kiti cha enzi mamaye mfalme; naye akaketi mkono wake wa kulia.