Eliya akamtwaa mtoto, akamchukua toka ghorofani mpaka chini ya nyumba ile, akampa mama yake. Eliya akanena, Tazama, mwanao yu hai.
1 Wafalme 17:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi la Elia; mtoto akaanza kupumua tena. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi la Elia; mtoto akaanza kupumua tena. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi la Elia; mtoto akaanza kupumua tena. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu akasikia kilio cha Ilya, na roho ya kijana ikamrudia, naye akafufuka. Neno: Maandiko Matakatifu bwana akasikia kilio cha Ilya, na roho ya kijana ikamrudia, naye akafufuka. BIBLIA KISWAHILI BWANA akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka. |
Eliya akamtwaa mtoto, akamchukua toka ghorofani mpaka chini ya nyumba ile, akampa mama yake. Eliya akanena, Tazama, mwanao yu hai.
Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu.
Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka.
Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.
Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,
Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;
Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama kwa miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.