1 Wafalme 15:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi, Asa akafanya yaliyo mema machoni pa Mungu, kama alivyofanya babaye Daudi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfalme Asa alitenda yaliyo mema mbele ya Mwenyezi-Mungu kama alivyofanya Daudi babu yake. Biblia Habari Njema - BHND Mfalme Asa alitenda yaliyo mema mbele ya Mwenyezi-Mungu kama alivyofanya Daudi babu yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfalme Asa alitenda yaliyo mema mbele ya Mwenyezi-Mungu kama alivyofanya Daudi babu yake. Neno: Bibilia Takatifu Asa akatenda yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, kama alivyokuwa ametenda Daudi, baba yake. Neno: Maandiko Matakatifu Asa akatenda yaliyo mema machoni mwa bwana, kama alivyokuwa ametenda Daudi baba yake. BIBLIA KISWAHILI Basi, Asa akafanya yaliyo mema machoni pa Mungu, kama alivyofanya babaye Daudi. |
Akaziendea dhambi zote za babaye, alizozifanya kabla yake; wala moyo wake haukuwa mkamilifu na BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi babaye.
Akaiendea njia yote ya Asa babaye; wala hakugeuka, akifanya yaliyo mema machoni pa BWANA. Lakini mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa dhabihu wakafukiza uvumba katika mahali pa juu.
Sulemani naye akampenda BWANA, akienda katika amri za Daudi babaye, ila hutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.
Ila mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.
Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, ila si kama babaye Daudi; akafanya kama yote aliyoyafanya baba yake Yoashi.
Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, akaenda katika njia yote ya Daudi baba yake, wala hakugeuka upande wa kulia wala wa kushoto.
Basi Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi, akatawala Asa mwanawe mahali pake; katika siku zake nchi ikastarehe miaka kumi.
Naye Asa akamlilia BWANA, Mungu wake, akasema, BWANA, hapana kuliko wewe aliye wa kusaidia, kati yake yeye aliye hodari, na yeye asiye na nguvu; utusaidie, Ee BWANA, Mungu wetu; kwa kuwa sisi twakutegemea wewe, na kwa jina lako tumekuja juu ya jamii kubwa hii. Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu wetu, asikushinde mwanadamu.
Lakini mahali pa juu hapakuondolewa katika Israeli; ila moyo wake Asa ulikuwa mkamilifu siku zake zote.