Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

1 Wafalme 14:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

BWANA akamwambia Ahiya, Angalia, mkewe Yeroboamu anakuja akuulize mambo ya mwanawe; kwa maana ni mgonjwa; umwambie hivi na hivi; kwani itakuwa akiingia atajifanya kuwa mwanamke mwingine.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mwenyezi-Mungu alikuwa amekwisha mwambia Ahiya kwamba mke wa Yeroboamu alikuwa njiani, anakuja kumwuliza yatakayompata mwanawe mgonjwa, na jinsi atakavyomjibu. Mkewe Yeroboamu alipofika, alijisingizia kuwa mtu mwingine.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mwenyezi-Mungu alikuwa amekwisha mwambia Ahiya kwamba mke wa Yeroboamu alikuwa njiani, anakuja kumwuliza yatakayompata mwanawe mgonjwa, na jinsi atakavyomjibu. Mkewe Yeroboamu alipofika, alijisingizia kuwa mtu mwingine.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mwenyezi-Mungu alikuwa amekwisha mwambia Ahiya kwamba mke wa Yeroboamu alikuwa njiani, anakuja kumwuliza yatakayompata mwanawe mgonjwa, na jinsi atakavyomjibu. Mkewe Yeroboamu alipofika, alijisingizia kuwa mtu mwingine.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Lakini Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Ahiya, “Mke wa Yeroboamu anakuja kukuuliza kuhusu mwanawe, kwa kuwa ni mgonjwa, nawe utamjibu hivi na hivi. Atakapowasili, atajifanya kuwa ni mtu mwingine.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Lakini bwana alikuwa amemwambia Ahiya, “Mke wa Yeroboamu anakuja kukuuliza kuhusu mwanawe, kwa kuwa ni mgonjwa, nawe utamjibu hivi na hivi. Atakapowasili, atajifanya kuwa ni mtu mwingine.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

BWANA akamwambia Ahiya, Angalia, mkewe Yeroboamu anakuja akuulize mambo ya mwanawe; kwa maana ni mgonjwa; umwambie hivi na hivi; kwani itakuwa akiingia atajifanya kuwa mwanamke mwingine.

Tazama sura
Tafsiri zingine

1 Wafalme 14:5
8 Marejeleo ya Msalaba  

Yoabu akatuma watu waende Tekoa, akaleta kutoka huko mwanamke mwenye akili, akamwambia, Nakusihi, ujifanye kama unaomboleza, ukavae nguo za kufiwa, nakusihi, wala usijitie mafuta, ila ukafanane na mwanamke aliyeomboleza siku nyingi kwa ajili yake aliyefariki;

Ikawa, Ahiya alipoisikia sauti ya miguu yake, akiingia mlangoni, alisema, Karibu, mkewe Yeroboamu; mbona wajifanya kuwa mwingine maana nimetumwa kwako wewe, mwenye maneno mazito.

Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na BWANA amenificha, wala hakuniambia.

Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya BWANA.

Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.