Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alichuma matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
1 Wafalme 13:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi mtu yule akarudi pamoja naye, akala chakula, akanywa maji nyumbani mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, mtu wa Mungu akarudi pamoja naye, akala chakula na kunywa maji kwa huyo mzee. Biblia Habari Njema - BHND Basi, mtu wa Mungu akarudi pamoja naye, akala chakula na kunywa maji kwa huyo mzee. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, mtu wa Mungu akarudi pamoja naye, akala chakula na kunywa maji kwa huyo mzee. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo mtu wa Mungu akarudi pamoja naye na akala na kunywa katika nyumba yake. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo mtu wa Mungu akarudi pamoja naye na akala na kunywa katika nyumba yake. BIBLIA KISWAHILI Basi mtu yule akarudi pamoja naye, akala chakula, akanywa maji nyumbani mwake. |
Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alichuma matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la BWANA, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.
Hata ikawa, walipokuwa wameketi mezani, neno la BWANA likamjia nabii yule aliyemrudisha;
maana ndivyo nilivyoagizwa kwa neno la BWANA, kusema, Usile chakula chochote wala usinywe maji, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia.
Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kama ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;
wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya BWANA, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru BWANA, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako.
Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.