na Adoramu alikuwa akiwaongoza Shokoa; na Yehoshafati, mwana wa Ahiludi, alikuwa mwekaji kumbukumbu;
1 Wafalme 12:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo mfalme Rehoboamu akampeleka Adoramu, aliyekuwa juu ya shokoa, nao Israeli wote wakampiga kwa mawe hata akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda katika gari, ili akimbilie Yerusalemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfalme Rehoboamu alipomtuma Adoramu, aliyekuwa mnyapara mkuu wa kazi za kulazimishwa, watu wote wa Israeli walimpiga mawe, wakamuua. Naye Rehoboamu alipanda haraka gari lake la kukokotwa, akakimbilia Yerusalemu. Biblia Habari Njema - BHND Mfalme Rehoboamu alipomtuma Adoramu, aliyekuwa mnyapara mkuu wa kazi za kulazimishwa, watu wote wa Israeli walimpiga mawe, wakamuua. Naye Rehoboamu alipanda haraka gari lake la kukokotwa, akakimbilia Yerusalemu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfalme Rehoboamu alipomtuma Adoramu, aliyekuwa mnyapara mkuu wa kazi za kulazimishwa, watu wote wa Israeli walimpiga mawe, wakamuua. Naye Rehoboamu alipanda haraka gari lake la kukokotwa, akakimbilia Yerusalemu. Neno: Bibilia Takatifu Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, aliyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu, akafanikiwa kuingia kwenye gari lake la vita na kutorokea Yerusalemu. Neno: Maandiko Matakatifu Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, aliyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu, akafanikiwa kuingia kwenye gari lake na kutorokea Yerusalemu. BIBLIA KISWAHILI Ndipo mfalme Rehoboamu akampeleka Adoramu, aliyekuwa juu ya shokoa, nao Israeli wote wakampiga kwa mawe hata akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda katika gari, ili akimbilie Yerusalemu. |
na Adoramu alikuwa akiwaongoza Shokoa; na Yehoshafati, mwana wa Ahiludi, alikuwa mwekaji kumbukumbu;
Na Ahishari alikuwa mkuu wa kasri; na Adoramu mwana wa Abda alikuwa msimamizi wa shokoa.
Akatuma watu elfu kumi huko Lebanoni kwa zamu kila mwezi. Mwezi mmoja walikaa huko Lebanoni na miezi miwili walikuweko nyumbani kwao. Na Adoramu alikuwa msimamizi wa shokoa.
Ndipo mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, msimamizi wa shokoa; nao wana wa Israeli wakampiga kwa mawe hadi akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda garini mwake, ili akimbilie Yerusalemu.
Basi, wakafanya shauri juu yake, wakampiga kwa mawe kwa amri ya mfalme katika ua wa nyumba ya BWANA.
Musa akamlilia BWANA, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe.
Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa BWANA ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote.
Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe.