Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wote wa dunia.
1 Wafalme 10:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo, mfalme Solomoni aliwapita wafalme wote duniani kwa mali na hekima. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo, mfalme Solomoni aliwapita wafalme wote duniani kwa mali na hekima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo, mfalme Solomoni aliwapita wafalme wote duniani kwa mali na hekima. Neno: Bibilia Takatifu Mfalme Sulemani alikuwa na utajiri mkubwa na mwenye hekima kuliko wafalme wote wa dunia. Neno: Maandiko Matakatifu Mfalme Sulemani alikuwa mkuu zaidi kwa utajiri na hekima kuliko wafalme wote wa dunia. BIBLIA KISWAHILI Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima. |
Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wote wa dunia.
Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa.
Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; pia hekima yangu nikakaa nayo.
Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii ya kuwahubiria Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;