Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

1 Wafalme 1:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Ee mfalme, bwana wangu, macho ya Israeli wote yanakuelekea wewe, kwamba uwaambie ni nani atakayeketi katika kiti chako cha enzi baada yako, Ee mfalme, bwana wangu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Na sasa, bwana wangu mfalme, Waisraeli wote wanakungojea, ili uwaambie yule atakayeketi juu ya kiti chako baada yako, bwana wangu mfalme.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Na sasa, bwana wangu mfalme, Waisraeli wote wanakungojea, ili uwaambie yule atakayeketi juu ya kiti chako baada yako, bwana wangu mfalme.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Na sasa, bwana wangu mfalme, Waisraeli wote wanakungojea, ili uwaambie yule atakayeketi juu ya kiti chako baada yako, bwana wangu mfalme.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Bwana wangu mfalme, macho ya Israeli yote yanakutazama wewe wajue kutoka kwako kuwa ni nani atakayeketi kwenye kiti cha ufalme cha bwana wangu mfalme baada yake.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Bwana wangu mfalme, macho ya Israeli yote yanakutazama wewe wajue kutoka kwako kuwa ni nani atakayeketi katika kiti cha ufalme cha bwana wangu mfalme baada yake.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ee mfalme, bwana wangu, macho ya Israeli wote yanakuelekea wewe, kwamba uwaambie ni nani atakayeketi katika kiti chako cha enzi baada yako, Ee mfalme, bwana wangu.

Tazama sura
Tafsiri zingine

1 Wafalme 1:20
11 Marejeleo ya Msalaba  

Roho ya BWANA ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa ulimini mwangu.

Tena amechinja ng'ombe, na vinono, na kondoo tele, na kuwaita wana wa mfalme wote pia, na Abiathari, kuhani, na Yoabu, jemadari wa jeshi. Ila Sulemani, mtumishi wako, huyu hakumwita.

Ama sivyo itakuwa, bwana wangu mfalme atakapolala pamoja na baba zake, mimi na mwanangu Sulemani tutahesabiwa kuwa wahalifu.

Jihadhari basi; kwani BWANA amekuchagua wewe ili ujenge nyumba itakayokuwa mahali patakatifu; uwe hodari ukatende hivyo.

Kisha mfalme Daudi akawaambia kusanyiko lote, Sulemani mwanangu, ambaye Mungu amemchagua peke yake, angali ni mchanga bado na hana uzoefu, nayo kazi hii ni kubwa; kwani nyumba hii ya enzi si kwa mwanadamu, ila kwa BWANA, Mungu.

Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yanatazama kwako.

Kama vile macho ya watumishi Yanavyoutegemea mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Yanavyoutegemea mkono wa bimkubwa wake; Ndivyo macho yetu yanavyomtegemea BWANA, Mungu wetu, Hadi atakapoturehemu.

Macho yangu humwelekea BWANA daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.

Maana, litazame jiwe hili nililoliweka mbele ya Yoshua; katika jiwe moja ziko nyuso saba; tazama, nitachonga maandishi yake, asema BWANA wa majeshi, nami nitauondoa uovu wa nchi hii katika siku moja.