Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;
1 Timotheo 6:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo basi, kama tunacho chakula na mavazi, tunapaswa kuridhika navyo. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo basi, kama tunacho chakula na mavazi, tunapaswa kuridhika navyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo basi, kama tunacho chakula na mavazi, tunapaswa kuridhika navyo. Neno: Bibilia Takatifu Lakini kama tuna chakula na mavazi, tutaridhika navyo. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini kama tuna chakula na mavazi, tutaridhika navyo. BIBLIA KISWAHILI ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. |
Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;
Akambariki Yusufu, akasema, Mungu ambaye baba zangu, Abrahamu na Isaka, walienenda mbele zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo,
Kwa kuwa BWANA, Mungu wako, amekubariki katika kazi yote ya mkono wako; amejua ulivyotembea katika jangwa kubwa hili; miaka arubaini hii alikuwa nawe BWANA, Mungu wako; hukukosa kitu.
Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yoyote niliyo nayo.