Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, au ulipizwe uovu kwa ajili yake
1 Timotheo 5:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale wanaotenda dhambi waonye hadharani, ili wengine wapate kuogopa. Biblia Habari Njema - BHND Wale wanaotenda dhambi waonye hadharani, ili wengine wapate kuogopa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale wanaotenda dhambi waonye hadharani, ili wengine wapate kuogopa. Neno: Bibilia Takatifu Wale wanaodumu katika dhambi uwakemee hadharani, ili wengine wapate kuogopa. Neno: Maandiko Matakatifu Wale wanaodumu katika dhambi uwakemee hadharani, ili wengine wapate kuogopa. BIBLIA KISWAHILI Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope. |
Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, au ulipizwe uovu kwa ajili yake
Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wagiriki waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa.
Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.
Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii gani ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi! Kwa kila njia mmejionesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.
Wanaume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.
Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.
lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
Ushuhuda huo ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali, ili wapate kuwa wazima katika imani;