Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.
1 Timotheo 5:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa maana wajane wengine wamekwisha potoka na kumfuata Shetani. Biblia Habari Njema - BHND Kwa maana wajane wengine wamekwisha potoka na kumfuata Shetani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa maana wajane wengine wamekwisha potoka na kumfuata Shetani. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana kwa kweli wajane wengine wamepotoka ili kumfuata Shetani. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana kwa kweli wajane wengine wamepotoka ili kumfuata Shetani. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani. |
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.
Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.
Waijua habari hii, ya kuwa wote walio wa Asia waliniepuka, ambao miongoni mwao wamo Figelo na Hermogene.
waliopotoka kutoka kwenye kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha tokea, hata kuipindua imani ya watu kadhaa.
Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia.
akisema juu ya mambo haya kama afanyavyo katika barua zake zote pia, katika barua hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuyaelewa na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wapotoavyo Maandiko mengine, na kujiletea maangamizi wao wenyewe.
Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.
Lile joka kuu likatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika wake wakatupwa pamoja naye.