Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
1 Timotheo 2:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanawake wanapaswa kukaa kimya na kuwa wanyenyekevu wakati wa kujifunza. Biblia Habari Njema - BHND Wanawake wanapaswa kukaa kimya na kuwa wanyenyekevu wakati wa kujifunza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanawake wanapaswa kukaa kimya na kuwa wanyenyekevu wakati wa kujifunza. Neno: Bibilia Takatifu Mwanamke na ajifunze katika utulivu na utiifu wote. Neno: Maandiko Matakatifu Mwanamke na ajifunze kwa utulivu na kwa utiifu wote. BIBLIA KISWAHILI Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. |
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Basi mbiu ya mfalme atakayoipiga itakapotangazwa katika ufalme wake wote, nao ni mkubwa, wake wote watawaheshimu waume zao, wakubwa kwa wadogo.
Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.
na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.
Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;