Balaamu akamwambia malaika wa BWANA, Nimefanya dhambi; maana sikujua ya kuwa wewe umesimama njiani ili kunipinga; basi sasa, ikiwa umechukizwa, nitarudi tena.
1 Samueli 29:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi sasa rudi, uende zako kwa amani, ili usiwachukize hao wakuu wa Wafilisti. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo sasa, rudi nyumbani. Nenda kwa amani ili usiwachukize wakuu wa Wafilisti.” Biblia Habari Njema - BHND Hivyo sasa, rudi nyumbani. Nenda kwa amani ili usiwachukize wakuu wa Wafilisti.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo sasa, rudi nyumbani. Nenda kwa amani ili usiwachukize wakuu wa Wafilisti.” Neno: Bibilia Takatifu Rudi na uende kwa amani; usifanye chochote cha kuwakasirisha watawala wa Wafilisti.” Neno: Maandiko Matakatifu Rudi na uende kwa amani; usifanye chochote cha kuwakasirisha watawala wa Kifilisti.” BIBLIA KISWAHILI Basi sasa rudi, uende zako kwa amani, ili usiwachukize hao wakuu wa Wafilisti. |
Balaamu akamwambia malaika wa BWANA, Nimefanya dhambi; maana sikujua ya kuwa wewe umesimama njiani ili kunipinga; basi sasa, ikiwa umechukizwa, nitarudi tena.
Ndipo Eli akajibu, akasema, Nenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.
Ndipo Akishi akamwita Daudi, akamwambia, Aishivyo BWANA, wewe umekuwa mwenye adili, tena kutoka kwako na kuingia kwako pamoja nami katika jeshi ni kwema machoni pangu; kwa sababu mimi sikuona uovu ndani yako tangu siku ile uliponijia hata leo; walakini hao wakuu hawakuridhii.
Naye Daudi akamwambia Akishi, Lakini mimi nimefanyaje? Nawe umeona nini kwangu mimi mtumishi wako, muda wote niliokaa mbele yako hata leo, nisipate ruhusa niende na kupigana na adui za bwana wangu mfalme?