Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.
1 Samueli 23:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye Daudi akakwea kutoka huko, akakaa katika ngome ya Engedi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Daudi aliondoka mahali hapo, akaenda kuishi kwenye ngome ya mji wa Engedi. Biblia Habari Njema - BHND Daudi aliondoka mahali hapo, akaenda kuishi kwenye ngome ya mji wa Engedi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Daudi aliondoka mahali hapo, akaenda kuishi kwenye ngome ya mji wa Engedi. Neno: Bibilia Takatifu Naye Daudi akakwea kutoka huko na kuishi katika ngome za En-Gedi. Neno: Maandiko Matakatifu Naye Daudi akakwea kutoka huko na kuishi katika ngome za En-Gedi. BIBLIA KISWAHILI Naye Daudi akakwea kutoka huko, akakaa katika ngome ya Engedi. |
Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.
Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng'ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio Engedi).
Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu nao; toka Engedi mpaka En-eglaimu, patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu; samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana.
Basi Sauli akarudi kutoka kumwinda Daudi, akaenda kupigana na Wafilisti; kwa hiyo wakapaita mahali pale, Selahamalekothi.
Ikawa, Sauli aliporudi baada ya kuwafuatia Wafilisti, aliambiwa ya kwamba, Daudi yuko katika nyika ya Engedi.
Naye Daudi akamwapia Sauli. Kisha Sauli akaenda zake kwao; lakini Daudi na watu wake wakapanda kwenda ngomeni.