1 Samueli 23:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Watu wa Keila watanitoa, nitiwe mkononi mwake? Je! Sauli atashuka, kama mtumishi wako alivyosikia? Ee Bwana, Mungu wa Israeli, nakusihi, umwambie mtumishi wako. Naye BWANA akamjibu, Atashuka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, wakazi wa Keila watanitia mikononi mwa Shauli? Je, Shauli atakuja kweli kama nilivyosikia mimi mtumishi wako? Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nakuomba unijibu mimi mtumishi wako.” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Shauli atakuja.” Biblia Habari Njema - BHND Je, wakazi wa Keila watanitia mikononi mwa Shauli? Je, Shauli atakuja kweli kama nilivyosikia mimi mtumishi wako? Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nakuomba unijibu mimi mtumishi wako.” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Shauli atakuja.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, wakazi wa Keila watanitia mikononi mwa Shauli? Je, Shauli atakuja kweli kama nilivyosikia mimi mtumishi wako? Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nakuomba unijibu mimi mtumishi wako.” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Shauli atakuja.” Neno: Bibilia Takatifu Je, watu wa Keila watanisalimisha kwake? Je, Sauli atateremka, kama mtumishi wako alivyosikia? Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, mwambie mtumishi wako.” Naye Mwenyezi Mungu akasema, “Ndiyo, atashuka.” Neno: Maandiko Matakatifu Je, watu wa Keila watanisalimisha kwake? Je, Sauli atateremka, kama mtumishi wako alivyosikia? Ee bwana, Mungu wa Israeli, mwambie mtumishi wako.” Naye bwana akasema, “Ndiyo, atashuka.” BIBLIA KISWAHILI Je! Watu wa Keila watanitoa, nitiwe mkononi mwake? Je! Sauli atashuka, kama mtumishi wako alivyosikia? Ee Bwana, Mungu wa Israeli, nakusihi, umwambie mtumishi wako. Naye BWANA akamjibu, Atashuka. |
Ndipo Daudi akasema, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, mimi mtumishi wako nimesikia hakika ya kuwa Sauli anataka kuja huku Keila, ili kuuharibu mji kwa ajili yangu.
Ndipo Daudi akasema, Je! Watu wa Keila watanitia mimi na watu wangu mkononi mwake Sauli? BWANA akasema, Watakutia.