Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii.
1 Samueli 20:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nawe utanionesha fadhili za BWANA, ili nisife, si wakati huu tu maadamu mimi ni hai; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ikiwa nitaendelea kuwa hai basi, nioneshe ule upendo thabiti wa Mwenyezi-Mungu, ili nisife, Biblia Habari Njema - BHND Ikiwa nitaendelea kuwa hai basi, nioneshe ule upendo thabiti wa Mwenyezi-Mungu, ili nisife, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ikiwa nitaendelea kuwa hai basi, nioneshe ule upendo thabiti wa Mwenyezi-Mungu, ili nisife, Neno: Bibilia Takatifu Lakini nitendee wema usiokoma kama ule wa Mwenyezi Mungu siku zote za maisha yangu, ili nisije nikauawa, Neno: Maandiko Matakatifu Lakini nitendee wema usiokoma kama ule wa bwana siku zote za maisha yangu, ili nisije nikauawa, BIBLIA KISWAHILI Nawe utanionesha fadhili za BWANA, ili nisife, si wakati huu tu maadamu mimi ni hai; |
Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii.
Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani?
Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu yeyote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu.
BWANA anitende mimi, Yonathani, hivyo, na kuzidi, ikiwa yampendeza babangu kukutenda mabaya, nisipokufunulia haya, na kukutuma uende zako kwa amani; na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.
lakini pamoja na hayo, hata jamaa yangu pia hutawaondolea kabisa fadhili zako; la, hata wakati ule BWANA atakapokuwa amewaondoa kabisa adui za Daudi wote pia katika uso wa nchi.
Na kwa habari ya neno lile tulilonena, wewe na mimi, angalia BWANA yu kati ya wewe na mimi milele.
Basi sasa, uniapie kwa BWANA, ya kwamba hutawakatilia mbali wazao wangu baada yangu, wala hutaliharibu jina langu katika ukoo wa baba yangu.