Ndipo Daudi akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa BWANA, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala.
1 Samueli 15:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye Sauli akamwabudu BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Samueli akarudi pamoja naye mpaka Gilgali na Shauli akamwabudu Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Samueli akarudi pamoja naye mpaka Gilgali na Shauli akamwabudu Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Samueli akarudi pamoja naye mpaka Gilgali na Shauli akamwabudu Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo Samweli akarudi pamoja na Sauli, naye Sauli akamwabudu Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo Samweli akarudi pamoja na Sauli, naye Sauli akamwabudu bwana. BIBLIA KISWAHILI Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye Sauli akamwabudu BWANA. |
Ndipo Daudi akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa BWANA, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala.
Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli.
Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu BWANA, Mungu wako.
Ndipo Samweli akasema, Nileteeni hapa Agagi, mfalme wa Waamaleki. Basi Agagi akamwendea kwa ulegevu. Naye Agagi akasema, Bila shaka uchungu wa mauti umeondoka.