Kutoka kwa damu yao waliouawa, Kutoka kwa shahamu yao mashujaa, Upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, Wala upanga wa Sauli haukurudi bure.
1 Samueli 14:48 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye kwa ushujaa, akawapiga Waamaleki, na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa mikono ya waliowateka nyara. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alipigana kwa uhodari, akawashinda Waamaleki. Aliwaokoa Waisraeli kutoka kwa watu wote waliowashambulia. Biblia Habari Njema - BHND Alipigana kwa uhodari, akawashinda Waamaleki. Aliwaokoa Waisraeli kutoka kwa watu wote waliowashambulia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alipigana kwa uhodari, akawashinda Waamaleki. Aliwaokoa Waisraeli kutoka kwa watu wote waliowashambulia. Neno: Bibilia Takatifu Akapigana kishujaa na kuwashinda Waamaleki, akiikomboa Israeli kutoka mikono ya wale waliokuwa wamewateka nyara. Neno: Maandiko Matakatifu Akapigana kishujaa na kuwashinda Waamaleki, akiikomboa Israeli kutoka mikono ya wale waliokuwa wamewateka nyara. BIBLIA KISWAHILI Naye kwa ushujaa, akawapiga Waamaleki, na kuwaokoa Waisraeli kutoka katika mikono ya waliowateka nyara. |
Kutoka kwa damu yao waliouawa, Kutoka kwa shahamu yao mashujaa, Upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, Wala upanga wa Sauli haukurudi bure.
BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.
Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha BWANA, Mungu wako, katika adui zako wote walio kandokando, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.