Ndipo wakuu wakamwendea Yeremia, wakamwuliza; naye akawaambia sawasawa na maneno aliyoamriwa na mfalme. Basi wakaacha kunena naye; maana neno lile halikujulikana.
1 Samueli 10:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Babaye mdogo Sauli akasema, Tafadhali niambie, huyo Samweli aliwaambiaje? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yule baba mdogo wa Shauli akamwambia, “Tafadhali, niambie kile alichokuambia Samueli.” Biblia Habari Njema - BHND Yule baba mdogo wa Shauli akamwambia, “Tafadhali, niambie kile alichokuambia Samueli.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yule baba mdogo wa Shauli akamwambia, “Tafadhali, niambie kile alichokuambia Samueli.” Neno: Bibilia Takatifu Babaye mdogo Sauli akasema, “Niambie Samweli amekuambia nini.” Neno: Maandiko Matakatifu Babaye mdogo Sauli akasema, “Niambie Samweli amekuambia nini.” BIBLIA KISWAHILI Babaye mdogo Sauli akasema, Tafadhali niambie, huyo Samweli aliwaambiaje? |
Ndipo wakuu wakamwendea Yeremia, wakamwuliza; naye akawaambia sawasawa na maneno aliyoamriwa na mfalme. Basi wakaacha kunena naye; maana neno lile halikujulikana.
Basi babaye mdogo akamwuliza Sauli na mtumishi wake, Je! Mlikwenda wapi? Naye akajibu, Tulikwenda ili kuwatafuta hao punda; na tulipoona ya kwamba hawakuonekana, tulimwendea Samweli.
Lakini Sauli akamjibu babaye mdogo, Alituambia waziwazi ya kuwa hao punda wamekwisha onekana. Lakini habari ya ufalme, ambayo Samweli alimwambia, hakuitaja.