1 Petro 5:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni. Biblia Habari Njema - BHND Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni. Neno: Bibilia Takatifu Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye anajishughulisha sana na mambo yenu. Neno: Maandiko Matakatifu Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu. BIBLIA KISWAHILI huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. |
Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.
Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?
Akawaambia wanafunzi wake, Kwa sababu hiyo nawaambia, Msisumbukie maisha yenu, mtakula nini; wala miili yenu, mtavaa nini.
Basi, ikiwa hamwezi hata neno lililo dogo, kwa nini kujisumbua kwa ajili ya yale mengine?
Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.