Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi sawa na hayo?
1 Petro 5:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Salimianeni kwa busu la upendo. Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. Amina. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Salimianeni kwa ishara ya upendo wa Kikristo. Nawatakieni amani nyinyi mlio wake Kristo. Biblia Habari Njema - BHND Salimianeni kwa ishara ya upendo wa Kikristo. Nawatakieni amani nyinyi mlio wake Kristo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Salimianeni kwa ishara ya upendo wa Kikristo. Nawatakieni amani nyinyi mlio wake Kristo. Neno: Bibilia Takatifu Salimianeni kwa busu la upendo. Amani iwe nanyi nyote mlio katika Al-Masihi. Neno: Maandiko Matakatifu Salimianeni kwa busu la upendo. Amani iwe nanyi nyote mlio katika Al-Masihi. BIBLIA KISWAHILI Salimianeni kwa busu la upendo. Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. Amina. |
Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi sawa na hayo?
Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu.
kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.
Amani na iwe kwa ndugu, na upendo, pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo.
kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.