1 Petro 3:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni nani atakayeweza kuwadhuru nyinyi kama mkizingatia kutenda mema? Biblia Habari Njema - BHND Ni nani atakayeweza kuwadhuru nyinyi kama mkizingatia kutenda mema? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni nani atakayeweza kuwadhuru nyinyi kama mkizingatia kutenda mema? Neno: Bibilia Takatifu Basi, ni nani atakayewadhuru mkiwa wenye juhudi katika kutenda mema? Neno: Maandiko Matakatifu Basi, ni nani atakayewadhuru mkiwa wenye juhudi katika kutenda mema? BIBLIA KISWAHILI Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema? |
Mtwae, umtunze sana, wala usimtende neno baya lolote; lakini umtendee kama atakavyokuambia.
Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake;
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Ufuatilieni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kutoa unabii.
Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
na awe ameshuhudiwa kwa matendo mema; katika kulea watoto, kuwa mkaribishaji, kuwaosha watakatifu miguu, kuwasaidia wateswao, na kujitolea kutenda wema katika hali zote.
ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.
Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.