BWANA akamwambia, Mataifa mawili yako tumboni mwako, Na makabila mawili ya watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.
1 Mambo ya Nyakati 5:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hawa ndio wazawa wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli. (Ingawa Reubeni alikuwa mzaliwa wa kwanza haki yake ya mzaliwa wa kwanza ilipewa Yosefu nduguye kwa sababu Reubeni alilala na suria wa baba yake. Hivyo, yeye hakutiwa katika orodha ya ukoo kulingana na haki yake ya mzaliwa wa kwanza. Biblia Habari Njema - BHND Hawa ndio wazawa wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli. (Ingawa Reubeni alikuwa mzaliwa wa kwanza haki yake ya mzaliwa wa kwanza ilipewa Yosefu nduguye kwa sababu Reubeni alilala na suria wa baba yake. Hivyo, yeye hakutiwa katika orodha ya ukoo kulingana na haki yake ya mzaliwa wa kwanza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hawa ndio wazawa wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli. (Ingawa Reubeni alikuwa mzaliwa wa kwanza haki yake ya mzaliwa wa kwanza ilipewa Yosefu nduguye kwa sababu Reubeni alilala na suria wa baba yake. Hivyo, yeye hakutiwa katika orodha ya ukoo kulingana na haki yake ya mzaliwa wa kwanza. Neno: Bibilia Takatifu Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu mwana wa Israeli. Hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa. Neno: Maandiko Matakatifu Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu mwana wa Israeli. Hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa. BIBLIA KISWAHILI Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza. |
BWANA akamwambia, Mataifa mawili yako tumboni mwako, Na makabila mawili ya watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.
Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa BWANA ameona mateso yangu; sasa mume wangu atanipenda.
Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari. Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.
Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli walioingia Misri, Yakobo na wanawe: Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo.
Basi sasa wanao wawili uliozaliwa katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni.
Hawa ndio wana wa Israeli; Reubeni, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni;
Hosa naye, wa wana wa Merari, alikuwa na wana; Shimri mkuu wao; (kwani ajapokuwa yeye si mzaliwa wa kwanza, babaye alimweka mkuu);
Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba zao: wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; ni Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi; hao ni jamaa za Reubeni.
Na mwanamume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni;
Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli, wana wa Reubeni; wa Hanoki, jamaa ya Wahanoki; na wa Palu, jamaa ya Wapalu;
Hakika habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.
lakini amkubali mzaliwa wa kwanza mwana wa yule asiyempenda, kwa kumpa mafungu mawili katika vyote alivyo navyo; kwa maana ndiye mwanzo wa nguvu zake; haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.
Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.
Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.
Wakati huo wana wa Yuda walimwendea Yoshua hapo Gilgali; na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi, akamwambia, Wewe wajua hilo neno BWANA alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu, katika habari zangu, na katika habari zako wewe, tulipokuwa katika Kadesh-barnea.