Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
1 Mambo ya Nyakati 4:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nilimzaa kwa huzuni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yabesi, aliyeheshimiwa kuliko ndugu zake wote. Mama yake alimpa jina la Yabesi kwa sababu alimzaa kwa maumivu. Biblia Habari Njema - BHND Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yabesi, aliyeheshimiwa kuliko ndugu zake wote. Mama yake alimpa jina la Yabesi kwa sababu alimzaa kwa maumivu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yabesi, aliyeheshimiwa kuliko ndugu zake wote. Mama yake alimpa jina la Yabesi kwa sababu alimzaa kwa maumivu. Neno: Bibilia Takatifu Yabesi aliheshimiwa kuliko ndugu zake. Mama yake alimwita Yabesi, akisema, “Nilimzaa kwa huzuni.” Neno: Maandiko Matakatifu Yabesi aliheshimiwa kuliko ndugu zake. Mama yake alimwita Yabesi, akisema, “Nilimzaa kwa huzuni.” BIBLIA KISWAHILI Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nilimzaa kwa huzuni. |
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Na yule kijana hakukawia kulifanya neno lile, maana amependezewa na binti Yakobo, naye alikuwa mwenye heshima kuliko wote nyumbani mwa babaye.
Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.
Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
Naye akamwingilia mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana, akamwita jina lake Beria, kwa sababu maafa yalikuwa yameipata nyumba yake.
Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na makabila ya watu kwa ajili ya maisha yako.
Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa hamu kuu, wakayachunguza Maandiko kila siku, ili waone kama mambo hayo ndivyo yalivyo.
Akamwita mtoto, Ikabodi, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.