1 Mambo ya Nyakati 4:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, babaye Bethlehemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Penueli aliwazaa Gedori na Ezeri, na Ezeri akamzaa Husha. Hao ndio wazawa wa Huri mzaliwa wa kwanza wa Efratha, baba yake Bethlehemu. Biblia Habari Njema - BHND Penueli aliwazaa Gedori na Ezeri, na Ezeri akamzaa Husha. Hao ndio wazawa wa Huri mzaliwa wa kwanza wa Efratha, baba yake Bethlehemu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Penueli aliwazaa Gedori na Ezeri, na Ezeri akamzaa Husha. Hao ndio wazawa wa Huri mzaliwa wa kwanza wa Efratha, baba yake Bethlehemu. Neno: Bibilia Takatifu Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha. Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, na baba yake Bethlehemu. Neno: Maandiko Matakatifu Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha. Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na baba yake Bethlehemu. BIBLIA KISWAHILI na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, babaye Bethlehemu. |
Hao walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata; Shobali, babaye Kiriath-Yearimu;
Na wana wa Salma; Bethlehemu, na Wanetofathi, Atroth-beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi, na Wazori.
Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa.
Na hawa ndio wana wa babaye Etamu; Yezreeli, na Ishma, na Idbashi; na dada yao aliitwa jina lake Haselelponi;
Basi wakaenda mpaka maingilio ya Gedori, naam, mpaka upande wa mashariki wa bonde hilo, ili kuwatafutia kondoo wao malisho.
Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.