1 Mambo ya Nyakati 4:39 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi wakaenda mpaka maingilio ya Gedori, naam, mpaka upande wa mashariki wa bonde hilo, ili kuwatafutia kondoo wao malisho. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walienea hadi kwenye lango la mji wa Gedori, upande wa mashariki wa bonde, ili kuwatafutia kondoo wao malisho. Biblia Habari Njema - BHND Walienea hadi kwenye lango la mji wa Gedori, upande wa mashariki wa bonde, ili kuwatafutia kondoo wao malisho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walienea hadi kwenye lango la mji wa Gedori, upande wa mashariki wa bonde, ili kuwatafutia kondoo wao malisho. Neno: Bibilia Takatifu wakaenea wakafika viunga vya Gedori kuelekea mashariki mwa bonde wakitafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao. Neno: Maandiko Matakatifu wakaenea mpaka kwenye viunga vya Gedori kuelekea mashariki mwa bonde wakitafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao. BIBLIA KISWAHILI Basi wakaenda mpaka maingilio ya Gedori, naam, mpaka upande wa mashariki wa bonde hilo, ili kuwatafutia kondoo wao malisho. |
Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa.
hao waliotajwa majina yao ndio waliokuwa wakuu katika jamaa zao; na koo za baba zao zikaongezeka sana.
na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, babaye Bethlehemu.
Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu.