1 Mambo ya Nyakati 4:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi. Huyu alimzalia Yeredi, mwanzilishi wa Mji wa Gedori, Heberi, mwanzilishi wa mji wa Soko, na Yekuthieli, mwanzilishi wa Mji wa Zanoa. Biblia Habari Njema - BHND Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi. Huyu alimzalia Yeredi, mwanzilishi wa Mji wa Gedori, Heberi, mwanzilishi wa mji wa Soko, na Yekuthieli, mwanzilishi wa Mji wa Zanoa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi. Huyu alimzalia Yeredi, mwanzilishi wa Mji wa Gedori, Heberi, mwanzilishi wa mji wa Soko, na Yekuthieli, mwanzilishi wa Mji wa Zanoa. Neno: Bibilia Takatifu Hawa walikuwa watoto wa Bithia binti Farao, ambaye Meredi alikuwa amemwoa. Meredi alikuwa na mke mwingine wa kabila la Yuda ambaye aliwazaa: Yeredi baba wa Gedori, Heberi baba wa Soko, na Yekuthieli baba wa Zanoa. Neno: Maandiko Matakatifu Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi ambaye aliwazaa: Yeredi baba wa Gedori, Heberi baba wa Soko na Yekuthieli baba wa Zanoa. Hawa walikuwa watoto wa Bithia binti Farao, ambaye Meredi alikuwa amemwoa. BIBLIA KISWAHILI Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa. |
Na wana wa Kalebu, nduguye Yerameeli, walikuwa Mesha, mzaliwa wake wa kwanza, aliyekuwa babaye Zifu; na wana wa Maresha, babaye Hebroni.
Na wana wa Ezrahi; Yetheri, na Meredi, na Eferi, na Yaloni; na Miriamu akamzalia na Shamai, na Ishba, babaye Eshtemoa.
Na wana wa mkewe Hodia, dada yake Nahamu, walikuwa babaye Keila, Mgarmi, na Eshtemoa, Mmaaka.
Basi wakaenda mpaka maingilio ya Gedori, naam, mpaka upande wa mashariki wa bonde hilo, ili kuwatafutia kondoo wao malisho.
na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, babaye Bethlehemu.