Akawachukua mateka watu wa Yerusalemu wote pia, na wakuu wote, na mashujaa wote, watu elfu kumi; na mafundi wote, na wafua chuma wote; hapana mtu aliyebaki, ila waliokuwa wanyonge wa watu wa nchi.
1 Mambo ya Nyakati 4:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na Meonothai akamzaa Ofra; na Seraya akamzaa Yoabu, babaye Ge-harashimu; kwani hao walikuwa mafundi stadi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Meonothai alimzaa Ofra. Seraya alimzaa Yoabu, mwanzilishi wa Bonde la Mafundi, lililopewa jina hilo kwa sababu wote waliokuwa humo walikuwa mafundi stadi. Biblia Habari Njema - BHND Meonothai alimzaa Ofra. Seraya alimzaa Yoabu, mwanzilishi wa Bonde la Mafundi, lililopewa jina hilo kwa sababu wote waliokuwa humo walikuwa mafundi stadi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Meonothai alimzaa Ofra. Seraya alimzaa Yoabu, mwanzilishi wa Bonde la Mafundi, lililopewa jina hilo kwa sababu wote waliokuwa humo walikuwa mafundi stadi. Neno: Bibilia Takatifu Meonothai akamzaa Ofra. Seraya akamzaa Yoabu, baba wa Ge-Harashimu, lililoitwa hivyo kwa sababu watu walioishi humo walikuwa mafundi stadi. Neno: Maandiko Matakatifu Meonathai akamzaa Ofra. Seraya akamzaa Yoabu, baba wa Ge-Harashimu. Liliitwa hivyo kwa sababu watu walioishi humo walikuwa mafundi. BIBLIA KISWAHILI Na Meonothai akamzaa Ofra; na Seraya akamzaa Yoabu, babaye Ge-harashimu; kwani hao walikuwa mafundi stadi. |
Akawachukua mateka watu wa Yerusalemu wote pia, na wakuu wote, na mashujaa wote, watu elfu kumi; na mafundi wote, na wafua chuma wote; hapana mtu aliyebaki, ila waliokuwa wanyonge wa watu wa nchi.
Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake.