Naye Daudi akatuma mtu akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bathsheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?
1 Mambo ya Nyakati 3:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: Mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni. Biblia Habari Njema - BHND Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: Mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni. Neno: Bibilia Takatifu nao hawa ndio wana wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu: mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia wana wanne: Shamua, Shobabu, Nathani na Sulemani. Neno: Maandiko Matakatifu nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu: mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua, Shobabu, Nathani na Sulemani. BIBLIA KISWAHILI Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu; |
Naye Daudi akatuma mtu akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bathsheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?
Mfalme Sulemani akajibu, akamwambia mamaye, Na mbona wamtakia Adonia Abishagi, Mshunami? Umtakie na ufalme pia; kwa kuwa yeye ni ndugu yangu mkubwa; naam, umtakie yeye, na Abiathari kuhani, na Yoabu mwana wa Seruya.